UTUNZAJI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA
Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati hushirikiana idara zingine kutekeleza shughuli mtambuka zinazohusiana na utunzaji na usimamizi wa mazingira pamoja na udhibiti wa taka ngumu
1.1.Misitu ya Asili na upandaji miti
Katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Babati,kuna aina 2 za Misitu, ambazo ni misitu ya Hiafadhi ya Taifa na Misitu ya Vijiji. Misitu ya hifadhi ya Taifa ni 4 ambayo ni Msitu wa Bereko, Haraa, Ufiome na Msitu wa Nou.
Eneo lote la misitu katika mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya , linakadiriwa kuwa ni hekta 80,000. Kati ya hizo, hekta 25,871 ni misitu ya Hifadhi ya Taifa ambayo iko chini ya usimamizi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikisha jamii inayozunguka misitu hiyo. Jumla ya hekta 54,129 ni misitu iliyoko katika maeneo ya vijiji na inasimamiwa na vijiji husika. Miti ya asili inayopatikana katika misitu hiyo ni miti aina ya miombo ambayo inafaa kwa shughuli za ufugaji nyuki. Mbinu inayotumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika utekelezaji wa kampeni ya upandaji miti ni ushirikishwaji Jamii katika zoezi zima la kuikuza katika vtalu,kuipanda na pia kuitunza miti. Katika utaratibu huu ,Halmashauri inachangia nyenzo na ushauri wa kitaalam kwa watu wenye vitalu vya kaya, taasisi, vikundi na vitalu vya vijiji, ili wahusika wenyewe waweze kukuza miche ya miti katika vitalu vyao na kuipanda katika maeneo. Kila mwaka, lengo ni kupanda miti 1,500,000 na utekelezaji wake pamoja na kustawi kwa miti inayopandwa ni kati 70% hadi 85% kutegemeana na hali ya hewa ya mwaka husika.
1.2. Usafi wa Mazingira na udhibiti wa Taka ngumu na
Halmashauri ya Wilaya ya Babati inatekeleza sheria na. ya kufanya usafi wa mazingira kila jumamosi ya mwisho wa mwezi katika kata zote 25 zilizoko katika mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya. Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, viongozi na watendaji ngazi ya kata husimamia na kukagua usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ndani ya kata ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi,maeneo ya biashara, mazingira ya ofisi,minada na maeneo ya magulio. Maelekezo kwa kila kaya ni kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi licha ya kushiriki zoezi la jumla la mwisho wa mwezi. Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya amefungua jalada maalum la usafi wa mazingira wa kila mwezi kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za usafi wa mazingira za Kata kwa ajili ya uhakiki na ukaguzi wa kushutukiza katika maeneo yanayotolewa taarifa. Halmashauri pia inao mpango wa muda mrefu wa wa kujenga vizimba vya kudhibiti taka ngumu na kuanisha maeneo ya madampo yasiyopungua eka moja kwa kila eneo katika makao makuu ya Kata zenye idadi kubwa ya watu na zinaokua haraka kuelekea miji midogo. Kwa mwaka wa fedha 2016/17 Halmashauri ilitenga fedha kutokana na mapato ya ndani, na kuwezesha ujenzi wa vizimba 2 katka kata za Gallapo na Dareda na hivyo kuwa na jumla ya vizimba 3 na maeneneo yaliyoainishwa rasmi kama madampo ya kutupa taka ngazi ya Kata.
1.3 Shughuli nyingine za utekelezaji sheria Na.20 ya usimamizi wa mazingira mwaka 2004
Shughuli nyingine za mazingira zinazofanyika ni pamoja na:
2.0 Changamoto.
Fig 1. Uvunaji holela wa misitu
Fig 2. Uchungaji holela wa mifugo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.