UTARATIBU WA KUTOA LESENI
Leseni ya Biashara
Hiki ni kibali maalum cha Serikali kinachotolewa kwa mfanyabiashara yeyote anapotaka kufanya biashara hapa nchini. Sheria ya Leseni za Biashara Na. 25 ya 1972 – Kifungu cha 3(a) kimeweka bayana kuwa, Kibali hicho maalumu kinaitwa Leseni ya Biashara. Kwa hiyo basi, kufanya biashara yoyote bila kuwa na kibali hiki ni kosa la jinai.
Ili Mwombaji Apate Leseni Ya Biashara Anapaswa Kumbatanisha Nyaraka Zifuatazo:
· Nakala ya hati ya kuandikisha jina la Biashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract);
· “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa Kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao na utaifa wao;
· Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiri nje ya nchi ya Tanzania au hati ya kusafiri katika nchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (Affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania, na kama mgeni alete hati ya kuishi nchini daraja la kwanza (Residence Permit Class A).
· Endapo wenye hisa wote wapo nje ya nchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa mamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” zinazoainisha kuwa anasimamia kampuni husika.
· Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of occupancy, e.t.c);
· Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax Payer Identification Number - TIN).
Utaratibu Wa Kupewa Leseni:
Jaza fomu ya maombi ya Leseni (TFN 211 ya 2004)
· Ambatisha nyaraka kama ilivyoainishwa hapo juu kwa ajili ya ukaguzi (assessment) na kujulishwa kiasi cha ada cha kulipia;
· Kwa biashara za Kundi A, malipo yafanyike kupitia Benki ya NMB mahali popote kwa kutumia Akaunti Namba 412100671; Jina MDC ONW SOURCE
· Wasilisha “pay in slip” ya Benki ili kupata risiti halali ya Serikali;
Kupata Fomu hi bonyeza link hapo chini
FOMU YA MAOMBI YA BIASHARA.pdf
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.