Halmashauri ya wilaya ya Babati ina jumla ya hospitali mbili ikiwa ni hospitali ya Dareda na hospitali ya Bashnet, idadi ya vituo vya afya ni nane ikiwa kituo kimoja ni binafsi na vituo saba ni vya serikali, Jumla ya zahanati katika Halmashauri ya wilaya ya Babati ni arobaini ikiwa zahanati tano ni za binafsi na zahanati thelathini na tano ni za serikali, Halmashauri ya wilaya ya Babati inaendelea kuboresha huduma za afya kwa kuendeleza ujenzi wa vituo vya afya na kuondoa kero za wananchi kusafiri umbali mrefu kufata huduma za afya, Halmashauri ya wilaya ya Babati imepunguza vifo vya mama na mtoto kwa kutoa chanjo kwa wakati na kutoa elimu juu ya mama mjamzito kuhudhuria kliniki na kuepuka kujifungua kwa wakunga wa jadi. Halmashauri ya wilaya ya Babati imefanikiwa kuzuia magonjwa ya milipuko kwa kuhimiza ujenzi wa vyoo bora na kutoza faini kwa kaya zisizo na choo bora.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.