Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Joseph Mkirikiti amesisitiza Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kufanya kazi kwa pamoja,kujituma na kushirikiana ili kuwaletea maendeleo Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati . Mh. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo katika Mkutano wa ufunguzi wa Baraza jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Babati lililofanyika Leo Makao Makuu -Dareda " Nyinyi Madiwani bebeni hoja za Wananchi ili zijadiliwe kwenye Baraza na si Hoja za Mtu binafsi", amesisitiza Kiongozi huyo.Kila mnachokifanya kifanye kwa niaba ya Wananchi na Chama cha Mapinduzi kilichopo Madarakani. Aidha amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wote kwa kuchaguliwa na kuwashukuru Wananchi wote na Viongozi wa Dini kwa kuliombea Taifa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.