Baraza la Madiwani H/ Wilaya ya Babati wameishukuru serikali kuu kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo la Utawala Makao makuu ya H/ Wilaya ya Babati. Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa mara ya kwanza kwenye jengo jipya la H/Wilaya ya Babati lillilojengwa kijiji cha Endasago kata ya Arri " Sisi Baraza la Madiwani tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo jipya ambalo tumeanza kulitumia leo" amesisitiza kiongozi huyo . Mpaka sasa Serikali kuu imeishatoa fedha kiasi cha Tsh 2 billioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya H/Wilaya Babati. H/Wilaya ya Babati imehamia makao mapya kuanzia leo trh 3/8/2022.ambapo huduma zote zitapatika ktk ofisi hizo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.