Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga amewataka Watumishi na Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wasiogope kufika ofisini kwake wakati wowote endapo wamekutana na changamoto katika kutekeleza shughuli za serikali.Mkurugenzi Mtendaji ameyasema hayo leo kwenye kikao Maalum cha Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Babati kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati." Ofisi yangu iko wazi wakati wote kiongozi au mtumishi anakaribishwa kuleta ushauri,au changamoto na atasikilizwa" amesisitiza kiongozi huyo.Baraza la wafanyakazi pamoja na mambo mengine limepitia makisio ya mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka 2019/2020 na kupitisha makadirio ya Tsh 42,465,387,164.34 ikiwa ni Mapato ya ndani,Matumizi ya kawaida (0C), Mishahara na Miradi ya Maendeleo ili yaendelee kujadiliwa katika ngazi zinazofuata ili kupata bajeti nzuri itakayokidhi mahitaji ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.