Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Elizabeth Kitundu ameagiza Afisa Biashara,Watendaji wa Kata na Vijiji kuendelea kufuatilia Wafanyabiashara wanaouza sukari tofauti na bei elekezi ya Tsh 2700 kuwakamata kuwapeleka katika Vyombo vya sheria . Hayo ameyasema leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati liliofanyika makao Makuu ya Halmashauri Kata ya Dareda "Nimepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wananchi juu ya Wafanyabiashara kuuza sukari kwa bei ya juu kuliko maelekezo ya serikali, hivyo naagiza watendaji ngazi ya Vijiji kupita na kuwakamata Wafanyabiashara wanaoenda kinyume na maagizo ya Serikali." Amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo amewaomba wananchi wanaoishi karibu na Mbunga za Wanyama kutochukua sheria ya kuuwa Wanyama wanaotoka hifadhi za Wanyama kutokana na Mafuriko bali watoe taarifa ofisi za Mkurugenzi na Hifadhi ili kupata njia nzuri za kuwaondoa na kuwarudisha hifadhini.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.