Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Lazaro Twange ameagiza Watumishi na watoa huduma wote wanatoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kufanya kazi hiyo kwa kujituma, bidiii na uaminifu mkubwa . Mhe.Twange ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Afya ya Msingi kilichofanyika leo makao makuu ya H/ Wilaya ya Babati. " Kazi ya chanjo tuifanye kwa uaminifu na kwa wakati kwani saratani ya mlango wa kizazi inaathari kubwa kwa afya ya wanawake ulimwenguni kote" amesisitiza kiongozi huyo. Mhe Twange amesema changamoto zitakazojitokeza katika utekelezaji wa zoezi hili zitolewe taarifa na zitatuliwe kwa wakati ili zoezi hili likamilike kwa wakati. Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Dkt Hosea Madama amesema Zoezi la chanjo ya (HPV Vaccine)dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa kizazi inaanza leo tarehe 22.4 hadi 26.4.2024 na walengwa ni wasichana kuanzia miaka 9 had 14 wajitokeze kwa wingi
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.