Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange amewaomba wananchi wote kupeleka watoto kuanzia umri miezi 9 hadi miezi 59 kwenye vituo vya kutolea huduma au eneo lililotengwa kwenye vitongoji na vijiji kupata chanjo ya Surua/ Rubella. Mhe.Twange ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la H/ Wilaya ya Babati wakati akitoa taarifa ya Serikali kwenye Mkutano huo "Serikali imepanga kutoa chanjo ya Surua/ Rubella kuanzia tarehe 15-18/2/2024 hivyo kila mzazi mwenye mtoto mwenye umri huo ampeleke mtoto akapate chanjo hiyo" amesisitiza kiongozi huyo Wakati huo huo Mhe. Twange amesisitiza Madiwani na viongozi wengine kutenga siku kwenda katika maeneo yao ya kazi kusikilza na kutatua kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara,vikao na ziara mbalimbali za kikazi ili kupunguza manung'uniko ya wananchi kwa serikali yao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.