Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange ameagiza watu waliovamia eneo la Msitu wa asili wa Endaw ekari 192 katika kijiji Cha Endaw kata ya Qameyu kuhama haraka na kusitisha Shughuli zote huku akiutaka uongozi wa Kijiji hicho kurejesha fedha za wananchi waliouziwa maeneo ya kilimo Katika msitu.
DC Twange ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji hicho baada ya kuvamia eneo la hifandhi ya msitu na kuanzisha shughuli za kilimo ambapo ameagiza wananchi waliotoa fedha kupewa maeneo hayo warudushiwe fedha zao ndani ya wiki moja kuanzia leo Februari 17,2023, huku akiagiza Afisa mtendaji kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkurugenzi kwa ajili ya kuwaepusha wananchi kuingia kinyemela katika Msitu.
Twange amewataka Wananchi waliovamia msiti na kulima kwamba baada ya kumaliza shughuli za mavuno wahakikishe wanapanda miti waliyoikata Katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kurejesha ardhi hiyo kwa serikali ya Kijiji.
Ikumbukwe serikali imekuwa ikisisitiza Wananchi kupanda miti na kutunza Mazingira pamoja na kila Halmashauri nchini kupanda miti Milioni Moja na laki tano huku uharibifu wa misitu ukichangia kwa kiwango kikubwa kwa mabadiliko ya tabia nchi hivyo kupelekea mvua kuwa za kusuasua.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.