Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Babati kukamilisha miradi yote iliyotengewa fedha za nje na za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024 na kuanza kutoa huduma ifikapo Desemba 2024. Mhe. Twange ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la madiwani H/Wilaya ya Babati uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano. "Wahe. Madiwani na Watendaji naomba mpokee maagizo ya serikali na kwenda kutekeleza na kuhakikisha miradi imekamilika na kutoa huduma mwezi Desemba".Amesisitiza kiongozi huyo.Wakati huo huo Mhe. Twange ameomba madiwani kwenda kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa ajili ya kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenda daftari la kudumu la Wapiga kura litakalofanyika mwezi Septemba mwaka huu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.