Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange amewaomba madiwani wa Baraza la Madiwani H/Wilaya ya Babati kuendelea kuhamasisha na kuwajulisha wananchi umuhimu wa sensa katika maeneo yao. Mhe. Twange ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Sensa Wilaya ya Babati ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya serikali kwenye Baraza la Madiwani wa H/ Wilaya ya Babati lililofanyika ktk jengo jipya la H/ Wilaya kijiji cha Endasago Kata ya Arri " Madiwani ni wenyeviti wa kamati ya Sensa katika kata zao hivyo wanajukumu la kuhakikisha wanahamasisha wananchi" amesisitiza kiongozi huyo"Aidha amewaomba Madiwani kuhakikisha zoezi hilo linapita kwa amani na na usalama kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za uwepo wa viashiria vyote vya kupinga zoezi hili pamoja na kuwasaidia makarani kufanya kazi yao kwa ufanisi ktk maeneo yote ya kata.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.