Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange ameagiza Mhifadhi wa Mbuga ya Manyara kupita vijiji vilivyopakana na mbuga hiyo kutoa elimu ya kufukuza tembo kwa utaratibu ili kutoleta madhara na kuharibu mazao ya wananchi.Mhe Twange ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliofanyika katika kijiji cha Magara kata ya Magara H/ W ya Babati. " Piteni katika vijiji vinavyozunguka hifadhi toeni elimu dhidi ya kuwaondoa wanyama waharibifu kwa utaratibu bila kuleta madhara kwa wananchi" amesisitiza kiongozi huyo.Wakati huohuo ameagiza mhifadhi mkuu kuwa na mahusiano mema na wananchi wanapoitwa watoe ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa H/W Babati Anna Mbogo ameagiza Walimu wote wanaojitolea kufundisha kwa kufuata sheria kanuni na taratibu za ufundishaji zilizowekwa na serikali na kusikiliza wakuu wao wa kazi kwa ajili ya kuendeleza elimu.MheTwange ameongozana na meneja TANESCO,TARURA,RUWASA, Wakuu wa Idara na kutatua kero za wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.