Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti amesisitiza kuwa fedha zote zilizoletwa na Serikali kwa Mpango wa Elimu wa Kulipa kulingana na Matokeo(EP4R) zitumike kukamilisha madarasa yaliyoanzishwa na Wananchi na si vinginevyo. Mhe. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akitembelea na kukagua umaliziaji wa Maboma ya Madarasa ktk Shule za Sekondari za Kiru ,Gichameda na Matufa zilizoka ktk Halmashauri ya Wilaya ya Babati "Fedha hizi zimeletwa kusaidia jitihada za jamii kukamilisha madarasa yaliyanzishwa na wananchi zitumike kwa lengo lililokusudiwa na kwa wakati." amesisitiza Mkuu wa Mkoa .Aidha amewaagiza Watendaji wa Vijiji na Kata kutoa taarifa ya Mapato na Matumizi kwa wakati."Watendaji someni taarifa ya Mapato na matumizi kwa Wananchi ya fedha za zote zilizochangwa na Wananchi na fedha iliyoletwa na Mhe Rais. Amesisitiza Mhe. Mkuu wa Manyara.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.