Halmashauri ya Wilaya ya Babati imekisia kukusanya Kiasi cha Tsh. 46,644,001,298 kwa mwaka 2018/2019 kutoka vyanzo vya ndani,Ruzuku ya matumizi mengineyo,(OC), Mishahara ya Watumishi (PE) na kiasi cha Tsh 11,929,209,510 ni fedha za miradi ya Maendeleo.Akiwasilisha Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019 kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Ndg, Hamisi Idd Malinga, amesema,fedha nyingi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 zinategemewa kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo Vijijini Akichangia Bajeti hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Raymond Mushi amesisitiza fedha zitengwe kwa ajili ya kuhamasisha wananchi na Wawekezaji kujenga Viwanda ambayo ni Sera na Mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano. Wajumbe wa kikao hicho,wakichangia bajeti hiyo wamesisitiza miradi yote iliyotengewa fedha kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 iendelee kutengewa fedha kwa mwaka 2018/2019 mpaka ikamilike na kuanza kutoa huduma.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.