Mwenyekiti wa H/Wilaya ya Babati Mhe. Nicodemus Tarmo amewataka Wananchi wa Kata ya Kisangaji kuendelea kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ili watoto wao wapate elimu bora na kujiletea maendeleo .Mwenyekiti huyo ameyasema leo wakati akiongoza Kamati ya fedha Mipango na Uongozi kwenye ziara ya kutembekea na kukagua miradi mbalimbali kwenye Kata hiyo."Hapa shule ya sekondari ya Kisangaji tumeleta tsh 15,000,000 / fedha za mapato ya ndani ili zisaidie kukamilisha vyumba viwili vya madarasa,tunajua hazitoshi bali ongezeni nguvu zenu kukamilisha ujenzi huo" Amesisitiza kiongozi huyo. Amewaomba viongozi wa Kijiji na Kata kushirikiana na Wananchi kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.