Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo leo amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emanuela Kaganda kwenye Uzinduzi wa hamasa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27/11/2024 iliyofanyika Uwanja wa Mpira Kata ya Gallapo. Katika hotuba yake amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kugombea na kupiga kura ifikapo tarehe 27/11/2024. Aidha amewataka kipindi chote cha uchaguzi wananchi kuendelea kulinda amani , kudumisha upendo na ifikapo tarehe 27/11 /2024 wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Uzinduzi wa hamasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama, serikali na madhehebu ya dini na yametanguliwa na maombi kuliombea taifa kufanya uchaguzi wa amani
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.