Hospitali Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Babati imeamuliwa kujengwa Tarafa ya Mbugwe Kata ya Mwada Kijiji cha Mwada .Akisoma maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya RaisTamisemi kwenye Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati uliofanyika leo Makao ya H/Wilaya Kata ya Dareda , Mkuu wa Wilaya ya Babati kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara amesema amepokea Barua kutoka ofisi ya Rais Tamisemi inayoelekeza Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati itajengwa Kata ya Mwada kijiji cha Mwada.Baada ya Maelekezo hayo Mwenyekiti wa H/Wilaya ya Babati Mhe.Nicodemus Tarmo amewaomba wajumbe wa Mkutano huo kupokea maelekezo ya Waziri na kwenda kuyatekeleza kwani Mhe Waziri aliunda tume iliyo kuja na kutembelea maeneo yote na kuhoji viongozi na wataalam ambapo ilimpelekea taarifa Mhe Waziri na Majibu ndiyo hayo yaliyowasilishwa leo na Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.Awali Baraza la Madiwani lilipendekeza Hosipitali ya Halmashauri ijengwe Kata ya Arri Tarafa ya Bashnet.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.