Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya jamii. Dr. John Jingu ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kutenga na kutoa asilimia 10 kusaidia Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Dr. Jingu ameyasema hayo leo alipotembelea kikundi cha Wanawake cha Ereto kilichoko Kata ya Nkait, Kijiji cha Minjingu ktk Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kuona shughuli zinafanywa na kikundi hicho kilichokopeshwa na Halmashauri mwaka Jana kiasi cha Tsh 8,000,000/_ "Nawapongeza Halmashauri kwa kazi nzuri ya kutenga na kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia makundi maalum ya Wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu" Hii ni sheria pia Ilani ya Chama cha Mapinduzi inasisitiza Serikali kuwezesha Wananchi amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amewataka wanakikundi kufanya kazi kwa bidii kujituma ili kujiletea Maendeleo na jamii kwa ujumla.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.