Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi Maryam Muhaji leo ametembelea Kituo cha Afya Madunga H/Wilaya ya Babati na Kukagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto na jengo la kufulia ambapo ameagiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kata Madunga kukamilisha ujenzi huo ifikapo Mwezi Desemba Mwaka huu. Wakati huo huo Bi Muhaji amepongeza Wananchi na watumishi wa kituo cha Afya Madunga kwa utoaji huduma nzuri kwa wananchi .Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Bahati Anna Mbogo kwa niaba ya Wananchi wa Madunga ameshukuru serikali kuu kwa kutoa fedha kiasi cha Tsh 250,000,000/ katika ujenzi wa majengo hayo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.