Kikao cha Kamati ya Ushauri Wilaya ya Babati kimeshauri H/Wilaya ya Babati kuongeza juhudi za ukusanyaji mapato na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato.Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg Halfan Mathipula kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda katika ukumbi wa H/W wakati wa kujadili mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 "Halmashauri yaWilaya ya Babati inafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ongezeni bidii na anzisheni vyanzo vipya"amesisitiza kiongozi huyo.Wakati huo huo wajumbe wameshauri suala la ukusanyaji mapato yatokanayo na Chumvi kutoka ziwa Gidewari lipelekwe kwenye Kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa ili lijadiliwe upya H/ wilaya ya Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang waweze kupata mapato yatokanayo na ziwa hilo.H/Wilaya ya Babati inatarajia kukusanya, kupokea na kutumia kiasi cha Tshs 65.2 billion kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kulipa mishahara, kugharimia miradi ya maendeleo na matumizi mengine.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.