Halmashauri ya Wilaya Babati kwa msimu wa Kilimo wa mwaka 2019 imedhamilia kufanya vizuri katika kilimo cha Pamba na mazao mengine ya biashara ili wananchi wapate kipato kupitia Kilimo .Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Madiwani ya Uchumi ,Ujenzi na Mazingira Mhe Crescent Khaday katika kijiji cha Mwada kata ya Mwada wakati kamati hiyo ikikagua miradi ya maendeleo likiwemo Shamba la Pamba la Mkulima Ndg Rinus Mwacha (28) mkazi wa kijiji cha Mwada ambaye amelima Pamba Ekari 5."Halmashauri ya Wilaya ya Babati inawathamini Wakulima kwani wanachangia pato kubwa la Halmashauri yetu kwa mantiki hiyo sisi madiwani tunapita na kuhamasisha Wakulima walime mazao ya biashara yenye soko kama Pamba" amesisitiza kiongozi huyo.Katika hatua nyingine Kamati hiyo imekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Magugu kilichoko kijiji cha Magugu na kusisitiza Wasimamizi na Mafundi kuongeza nguvu katika ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo hicho.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.