Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Ndg Anna Mbogo anavitangazia Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu mikopo isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na H/ Wilaya. Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 H/Wilaya ya Babati imetenga fedha za Mapato ya ndani ya 10% kiasi cha Tsh 256,000,000/ kwa ajili ya kukopesha makundi hayo. Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa tarehe 25/7/2022 na Mkurugenzi kwenda kwa Watendaji kata na vijiji inaelekeza usajili na kutuma maombi unafanyika kwenye mfumo wa Electronic wa TPLMIS (https:mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz/login unaweza kutumia simu janja au komputa kuingia kwenye mfumo huo mahali na wakati wowote. Mkurugenzi Mtendaji amelekeza vikundi vya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kuanza sasa kutuma maombi kupitia mfumo huo. Mahitaji mengine ni kikundi kiwe na Email Address, kila mwanakikundi awe na namba za NIDA, namba ya simu, kikundi kiwe na Akaunt Bank. Wanavikundi wanasisitizwa kufika ofisi za Maendeleo ya jamiii zilizopo kwenye tarafa/kanda za Bashnet,Gorowa,MbugweAyalagaya na Babati au ofisi za kata kupata msaada zaidi wa kuomba mikopo ya Asilimia 10 isiyo na riba
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.