Maofisa Ugani wametakiwa kutoa ushauri stahiki ili wakulima walime kwa tija na ufanisi waweze kuongeza pato lao na kukuza uchumi wa nchi. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu leo kwenye Hafla fupi ya uzinduzi wa ununuzi wa zao lá Pamba kwa msimu wa mwaka 2018/2019 iliyofanyika kwenye viwanja vya chama chá Msingi Oridoy Kata ya Mwada Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mkuu wa Wilaya pia amewaeleza Wakulima na Wafanyabiashara kuwa kwa maelekezo ya Serikali mazao yatakusanywa na kuuzwa kupitia vyama vya Msingi na malipo ya fedha kwa kila Mkulima yatalipwa kupitia bank na hivyo kuwataka Wakulima kufunga akauti Bank. Chama chá Msingi Oridoy kwa msimu huu kitanunua Pamba Kwa kilo Tsh 1,100 kwa Pamba daraja la kwanza na daraja la Pili Tsh 600. Kabla ya uzinduzi wa Ununuzi wa Pamba Mhe. Mkuu wa Wilaya ametembelea Kiwanda cha kuchambu pamba chá Hanang Cotton Mill kilichopo kijiji cha Mawemairo Kata ya Magugu kinachomilikiwa na Mwekezaji Rajesh Atiya na kuona maandalizi ya uchambuzi wa Pamba kwa msimu mwaka 2018/2019.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.