June 13 2021 Mwenge wa uhuru umefanikiwa kupita wilayani Babati na kukagua miradi 3 ya maendeleo. Kiongozi wa mbio za mwenge 2021 Luteni Josephine Paul Mwampasho ameridhishwa na utekelezaji wa miradi yote 3, ikiwa ni pamoja na mradi wa Hospitali ya wilaya Mwada , ujenzi wa shule ya sekondari Ayalagaya na Mradi wa TEHAMA ujulikanao kama Government of Tanzania Health Management Information System (GoTHOMIS) katika Kituo cha Afya Magugu.
Mbio za mwenge mwaka 2021 zilizopambwa na kauli mbiu isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, itumike kwa usahihi na uwajibikaji" Kiongozi wa mbio za mwenge amesisitiza matumizi sahihi na salama ya TEHAMA katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwani matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua pato la Taifa na kurahisisha shughuli za kila siku.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.