Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Iddi Malinga ameagiza Wakuu wa Vituo na Zahanati kutoa huduma kwa ufanisi kwa Wananchi wote bila ubaguzi wowote hasa katika kipindi hiki dunia inapopambana na ugongwa hatari wa CORONA.Hayo ameyasema leo kwenye Kikao kazi cha wakuu wa Vituo na Zahanati wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kilichofanyoka Katika Ukumbi wa Halmashauri Mjini Babati."Msiwabague Wananchi kisa CORONA,toeni huduma nzuri kwa wananchi wote" amesisitiza Kiongizi huyo. Aidha Mkurugenzi Mtendaji amewashukuru Viongozi wa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kwa kushirikiana na Idara ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kuandaa kikao kazi hicho,”TALGWU mkoa wa Manyara mmekua mfano wa kuigwa, tumekua tukishirikiana pamoja katika kulinda na kutatua changamoto za watumishi wetu hasa kwa kipindi hiki kigumu cha ugonjwa hatari wa CORONA, Katibu wa TALGWU mkoa wa Manyara Ndg. Ndulila Pandauyage amewashukuru Mkurugenzi Mtendaji na Mganga Mkuu wa Wilaya kwa kutoa ushirikiano kukubali kushiriki pamoja kutoa Elimu kwa watumishi wa Afya kwani kazi ya chama ni kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira yasiyohatarisha afya za watumishi.Mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa wa TALGWU Mkoa wa Manyara Ndg Devotha Mbonamasabo amewasisitiza watumishi wenzake kufata kanuni,sheria na miongozo mbalimali ya utumishi wa umma, kusikiliza kwa makini na kufuata maelezo mbalimbali yanayotolewa kujikinga na kuwakinga wagomjwa wanaowahudumia kwani wenyewe ndio wanaotegemewa katika kutoa elimu katika vituo vyao vya kazi kujikinga na ugonjwa hatari wa CORONA
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.