Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo ameanzisha Kampeni ya Kupanda miti kwa kila taasisi zake ili kufikia lengo la kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka." Naagiza taasisi zote shule za Msingi, Sekondari, ofisi za vijiji na kata, vituo vya afya , zahanati, kupanda miti kuanzia sasa " amesisitiza kiongozi huyo. Akiwa anakagua leo upandaji miti katika eneo la Makao ya H/ Wilaya ameagiza Afisa Misitu kuhakikisha miche ya miti inaandaliwa haraka na inapandwa katika kipindi hiki cha mvua. Aidha ameomba wananchi nao wanaotaka kupanda miti wafike Halmashauri wamuone Afisa Misitu kwa ajili ya kupata miche ya miti.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.