Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewashukuru wafadhili wa Shirika la Karimu Foundation kwa ujenzi wa miradi ya sekta za Maji, Afya, Elimu na ujasilimari katika kata za Ayalagaya na Arri .Hayo ameyasema leo kwenye hafla iliyoandaliwa na wananchi wa kata za Arri na Ayalagaya ya kuwapongeza na kuwaaga kwa msimu huu iliyofanyika S/ Msingi Endasago Kijiji cha Endasago Kata ya Arri. " Tunatoa shukurani na pongezi nyingi kwa Karimu Foundation kwa kazi kubwa nzuri mliofanya asanteni sana na ushirikiano huo uendelee' amesisitiza kiongozi huyo. Mkurugenzi Mbogo amewaelekeza watendaji wa vijiji na kata hizi kusimamia na kuitunza miradi hiyo ili iwe endelevu na amehaidi kufanya ufuatiliaji wa kila mara kuhakikisha miradi hiyo inaendelezwa kwa ustawi wa wananchi wa kata za Arri na Ayalagaya. Shirika la Karim Foundation lenye makao Makuu kata ya Ayalagaya limekuwa mkombozi kwa kata za Arri na Ayalagaya kwa kufadhili miradi mbalimbali na kuwajengea uwezo wananchi ili wajitegemee.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.