Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya wametakiwa kuchangia shughuli.za maendeleo hasa ujenzi wa Zahanati na Shule ili kujiletea Maendeleo. Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga kwa nyakati tofauti akiwa Kijiji cha Gajal kata ya Ayalagaya akihamasisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Gajal pia akiwa Shule ya Sekondari ya Ayalagaya kata ya Ayalagaya akihamsisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na kupokea mradi wa ujenzi wa vyoo vya Wavulana matundu 12 Shule ya Sekondari Ayalagaya vilivyojengwa na Shirika la Karim International Help Fund ."Miradi hii inayojengwa ni yetu kwa maendeleo yetu ni lazima kila mmoja achangie kwa maendeleo yetu" Amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji.Akiwa zahanati ya Kijiji cha Gajal Mkurugenzi amechangia Bati 55 kwa ajili ya uapauzi wa Zahanati ya Kijiji hicho. Aidha Mkurugenzi Mtendaji amemshukuru Ndg Nelson Mattos Mfadhili Mkuu na Karim International kwa kwa ufadhili wao katika mradi wa ujenzi wa Vyoo Shule ya Sekondari ya Ayalagaya
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.