Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Lazaro Twange amesisitiza wananchi kuupenda na kuuenzi Muungano kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadae. Mhe. Twange ameyasema hayo leo kwenye zoezi la upandaji miti ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Aldersigate Babati Mjini."Kila mmoja anatakiwa Kushukuru Mungu Muungano wetu umefika miaka 60 upendeni Muungano huo".Amesisitiza kiongozi huyo.Wananchi na watumishi kutoka maeneo mbalimbali wameshiriki zoezi hilo la kupanda miti.Naye Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg.Halfan Matipula ametoa ratiba ya maadhimisho ya Sherehe hizo kuwa zoezi la upandaji miti na usafi wa mazingira litaendelea, na kutakuwa na Maombi ya kuliombea Taifa na Tamasha la michezo na Burudani litakalofanyika tarehe 25/4 na kusikiliza Hotuba ya Mhe. Rais kuanzia saa 3.00 usiku katika viwanja vya kwaraa maadhimisho yatafanyika 26/4. Katika Viwanja vya Kwaraa Mjini Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.