Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Muhaji amepongeza watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara kwa utoaji wa huduma nzuri. Hayo ameyasema leo katika hospitali hiyo kwenye ziara yake ya ukaguzi na ufuatiliaji wa miradi na kuangalia huduma zinazotolewa na miradi iliyojengwa na serikali. "Nawapongeza kwa utoaji wa huduma nzuri wagonjwa wamenihakikishia, endeleeni na Moyo huo" amesisitiza kiongozi huyo. Kwa upande wake Leila Rajabu ( Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji katika hospitali hapo) ameshukuru kwa huduma inayotolewa ktk hospital hiyo na kumueleza Katibu Tawala kuwa anashukuru Serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa Hospital nzuri na ya kisasa katika H/ Wilaya ya Babati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.