Mwekezaji anayemiliki Kampuni ya Republic Body Builders amerudisha shamba lake lenye ekari 1,098 kwa wananchi wa Kijiji cha Shaurimoyo kata ya Kisangaji Tarafa ya Mbugwe, Wilayani Babati Mkoa wa Manyara na kumaliza mgogoro kati yake na Wananchi wa Kijiji hicho uliodumu zaidi ya miaka 20.Shamba hilo lenye hati Na. 3264 Unit Na 2 limerudishwa kwa Wananchi kupitia Mkutano hadhara uliofanyika katika Kijiji hicho na kudhuliwa na umati wa wananchi, Diwani,Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Hamisi Malinga na Mwekezaji wa Kampuni hiyo.Kumalizika kwa Mgogoro huo ni jitihada za Mkuu wa Wilaya Mhe. Raymond Mushi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga wa kutatua kero na Migogoro ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.