Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wenye Ulemavu Shule ili wapate Elimu na ujuzi ili kujipatia kipato na kuendeleza Maisha yao. Hayo ameyasema Mhe. Stella Ikupa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu kwa nyakati tofauti alipotembelea kata za Gallapo na Magugu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati leo na kuongea na Watu wenye Ulemavu. "Wazazi wenye watoto wenye Ulemavu msiwafiche nendeni kwa Viongozi watawapa maelekezo ya kuwapeleka watoto wenye Ulemavu Shule, Msiwafiche," amesisitiza Mhe. Naibu Waziri .Katika Ziara hiyo Mhe Waziri amesisitiza Watu wenye Ulemavu kuunda vikundi ili waweze kukopesheka na fedha zitolewazo na Halmashauri kutoka mapato ya ndani za asilimia 2.Katika ziara hiyo amesikiliza kero za wananchi hasa Watu wenye Ulemavu na kuzitatua na Kusisitiza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwenda ngazi ya chini kutatua kero na Changamoto zinazowakabili watu wenye Ulemavu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.