Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe . Festo Dungange amewashukuru Wananchi wa Kata ya Mwada Wilaya ya Babati Kwa kutoa ardhi yenye hekari 70 Kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Babati . Mhe. Dungange ameyasema hayo leo katika Hospitali ya Halmashaurui ya Wilaya Mwada. kwenye ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi. " Nawashukuru Wananchi Kwa kutoa ardhi ya hekari 70 Kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali , ninachowaomba ardhi ilindwe isivamiwa na ipimwe ipate hati ya Umiliki" amesisitiza kiongozi huyo . Aidha amepongeza ubora wa majengo yanayojengwa na thamani ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa majengo ya Hospitali ya H/Wilaya ya Babati. Mhe. Naibu waziri ameagiza Ujenzi wa Wodi za Baba, Mama ,Watoto na nyumba ya Kuhifadhi maiti zikamilike kabla ya tarehe 30/5/2023. Katika ziara yake ameambatana na Viongozi mbalimbali ambapo Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ameshukuru Serikali Kwa kutoa fedha ujenzi wa Miradi katika Wilaya ya Babati na kuaidi maelekezo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.