Nyumba na Majengo yote ya Umma na Taasisi yaliyoko kwenye Vitongoji yatawekewa namba ya Anwani za Makazi. Akitoa taarifa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani H/ Wilaya ya Babati Mkurugenzi Mtendaji wa H /Wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema serikali imetoa maelekezo kuwa ifikapo mwezi Mei mwaka huu kuwa H/Wilaya ya Babati iwe imetekeleza mpango wa Mfumo wa Anwani za makazi ambapo kila nyumba na majengo ya taasisi yatawekewa namba za Anwani za Makazi. Mkurugenzi huyo amesema mfumo wa Anwani za makazi utakuwa na faida nyingi za kiuchumi na kijamii ikiwa ni kurahisisha upatikanaji, utoaji na upelekaji wa huduma za za bidhaa mahali stahiki,kila mtu anayeishi Tanzania atakuwa na Anwani halisi za Makazi na Usajili wa Mali, Biashara, vizazi na Vifo utaboreshwa.Katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji amewaomba Wahe. Madiwani kuanza kuhamasisha mpango huo, na Elimu nyingine itapelekwa vijijini na wataalam wake kuwafundisha na kuwahamasisha wananchi ngazi ya Kijiji na Kitongoji kuanza kutekeleza mpango huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.