Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga ameishukuru Kampuni Intracom fertilizers Limited kwa ujenzi wa Shule ya Msingi mpya ya Vilima vitatu. Shule hii imejengwa kata ya Nkait, kijiji cha Vilima vitatu Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo katika hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa shule hiyo uliofanyika katika shule ya Msingi mpya ya Vilima Vitatu "Mimi nawashukuru sana kampuni ya Itracom fertilizers na ninawakaribisha muendelee kuwekeza mkoa wa Manyara " amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo amemshukuru Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji. Mhe. Sendiga ameagiza uongozi wa kiwanda hicho kutangaza ajira zote wazi ili vijana wenye sifa waweze kuomba na kusisitiza kuwa wazawa wakipata ajira wataona faida za wawekezaji na watakuwa walinzi wa kiwanda hicho. Mwenyekiti wa Bodi ya Itracom Capt John Chiligati ameshukuru serikali kwa kukubali kampuni kuwekeza na akaomba shule hiyo itunzwe kwa maendeleo ya vizazi vijavyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.