Viongozi na Wananchi wa Kata ya Gallapo H/Wilaya ya Babati wameshauriwa kuongeza eneo la kituo cha Afya Gallapo kutoka ekari 7 za Sasa hadi kufikia ekari 10 na kuendelea ili waweze kujengewa majengo mapya ya Kituo cha Afya Gallapo. Naibu Waziri waTAMISEMI Mhe.Festo Dungange amesema leo ktk kituo Cha Afya Gallapo Ktk ziara yake ya kukagua Miradi Ktk H/ Wilaya " kituo hiki nimekifahamu muda mrefu kupitia kwa Mbunge wenu Daniel Sillo na leo nimekuja, katika ukaguzi wangu nimeambiwa kuna ekari 7 naomba muongeze angalau zifike10 ili Serikali ikileta fedha kujenga majengo ya Kisasa yote yaweze kuenea" amesisitiza kiongozi huyo. Awali akisoma taarifa kwa Naibu Waziri,Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dkt Nemael Sanka ameomba kituo hicho kujengewa majengo mapya na akasisitiza hasa ukamilishaji wa jengo la Upasuaji ambalo limejengwa na Wananchi wa Kata ya Gallapo Kwa kushirikiana na H/Wilaya ya Babati tangu 2019 mpaka Sasa halijakamilika.Mhe. Dungange amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano Kwa Serikali.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.