Wenyeviti pamoja na Makatibu wao katika vituo vya kutolea huduma za afya na Zahanati, Waganga wa vituo na zahanati na wahasibu wao wamehudhuria semina iliyotolewa na watumishi wa kada za afya,uhasibu naTEHAMA wa halimashauri ya Wilaya ya Babati katika ukumbi wa Halimashauri.Mafunzo haya yalihusisha iCHF iliyoboreshwa, JAZIA (Prime Vendor) mfumo huu unahusisha uagizaji wa dawa na vifaa tiba pale ambapo MSD imepungukiwa kutoa huduma ya dawa, mifumo mipya ya ya mfuko wa jamiii CLAIM MANAGEMENT pamoja na Acquire,mfumo wa kiuhasibu FFARS pia Mafunzo ya Direct Health Facility Financing katika ngazi za zahanati na Vituo vya Afya.Washiriki wa semina wamesisitizwa kutekeleza yale yote yaliyofundishwa ili kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi kwani serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na serikali inahakikisha fedha za huduma zinafika kwa wakati stahili.Katibu wa Afya wa halmashauri amewaomba washiriki kuzingatia mwongozo katika matumizi ya fedha kununua dawa na vifaa tiba kwa wakati na kila matumizi yanayofanywa yaingizwe kwenye mfumo wa FFARS ili kuleta takwimu sahihi na kuzuia hoja katika matumizi ya fedha.
Washiriki wamefurahia mafunzo wameipongeza serikali ya awamu ya tano na kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi mpaka ngazi za vijiji na kuiomba serikali kutoa mafunzo kama haya mara kwa mara ili kuongeza tija katika utendaji kazi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.