Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere ameagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara kuwa miundombinu yote ya Shule zinazojengwa iwekewe mifumo ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya shule. Kiongozi huyo ameyasema hayo leo ktk shule ya Sekondari Chief Dodo iliyoko Kata ya Riroda Tarafa ya Gorowa mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ktk shule hiyo kwenye siku ya pili ya ziara yake ktk H/ Wilaya ya Babati. "Shule nyingi zimejenga miundombinu mizuri lakini zina changamoto ya ukosefu wa Maji, ili kundoa changamoto hizo ni lazima mfumo wa uvunaji maji ya mvua ijengwe" amesisitiza kiongozi huyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.