Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu amesisitiza Vikundi vya Wanawake ,Vijana na Watu wenye ulemavu kutumia fedha wanazokopeshwa na Halmashauri kwa shughuli zilizokusudiwa ili waweze kujiletea maendeleo.Akitoa hundi ya Tsh 165,000,000 leo kwa vikundi 33 vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu vya H/Wilaya ya Babati katika hafla fupi ya kukabidhi hundi iliyofanyika katika ukumbi wa zamani wa H/Wilaya ya Babati , Mkuu wa Wilaya ya Babati amesisitiza fedha hizo wanazokopeshwa si ruzuku bali ni mkopo hivyo kila kikundi kinatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kurejesha fedha hizo kwa wakati
Matukio katika picha Mkuu wa wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri , Mkurugenzi pamoja na watendaji wengine wakipokea hundi kwa ajili ya mkopo wa vijana na watu wenye ulemavu
.Aidha ameagiza Halmashauri kuendelea kutenga na kutoa fedha za Mfuko wa Wanawake ,Vijana na Watu wenye ulemavu za asilimia 10 kwa mujibu wa Sheria.
Maafisa Utamaduni na vijana Bi Beatrice Mutsinzi pamoja na Bi Scholastika Mkumbi pamoja na Maafisa wa Maendeleo ya jamii wakifurahia ujio wa fedha hizo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.