Baraza la Madiwani la H/ Wilaya ya Babati limeagiza Watendaji wa Kata na Vijiji , Maofisa Elimu ngazi ya kata, Wakuu wa shule na walimu wakuu kuhakikisha wanafunzi wote sekondari waliochaguliwa kidato cha kwanza na waliondikishwa kuingia darasa la kwanza mwaka huu kuripoti shule haraka bila kikwazo chochote. Akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wakati wa kujadili taarifa za Kata, Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amesisitiza kila mzazi kuhakikisha anapeleka mtoto shule na kupokelewa bila kikwazo chochote." Sisi H/ Wilaya ya Babati hatuna upungufu wa madarasa hivyo ni lazima kila mzazi apeleke mtoto shule na apokelewe bila kikwazo chochote" amesisitiza kiongozi huyo na kuagiza serikali ngazi ya kata na Vijiji kusimamia agizo hilo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.