Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limeagiza Wananchi wanaotaka kuuza mahindi mabichi kuomba kibali cha kuuza Mahindi mabichi kuanzia sasa katika Ofisi za Watendaji wa Vijiji na Kata ili kulinda usalama wa chakula kwa muuzaji. Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mheshimiwa Nicodemus Tarmo Kwenye Mkutano wa Kwanza wa Baraza hilo wa kujadli taarifa za Kata uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ,Katika Mkutano huo baadhi Waheshimiwa Madiwani walitaka uuzaji wa mahindi mabichi usitishwe na wengine wakisema Wananchi waachiwe wakauze mahindi popote.Baada ya mjadala mrefu,ndipo ikaamuliwa Wananchi waruhusiwe kuuza Mahindi mabichi kwa kufuata utaratibu wa mwananchi kuomba kibali cha kuuza Mahindi mabichi Ofisi za Kata na Vijiji ili kulinda usalama wa chakula kwa muuzaji na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ujumla
Pia Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuweka Watendaji wa Vijiji katika Ofisi za Vijiji na Kata wanaoeleweka katika nafasi hizo ili kuharakisha ujenzi wa miradi ya Maendeleo na kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.Mkuu wa Wilaya ya Babati amesema hayo Leo kwenye Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kujadili taarifa za kata. "Ofisi za Vijiji na Kata ziwe na Watendaji wanaoeleweka hata kama akikaimishwa akaimishwe Mtendaji kwa Barua na awe mwadilifu hasa tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 amesisitiza kiongozi huyo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.