Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu amewapongeza Viongozi na Wananchi wa Vijiji vya Gallapo na Endanoga kata ya Gallapo kwa kujitokeza kwa wingi kuwasaidia wenzao waliopatwa na janga la upepo mkali kuezua nyumba na kujeruhi baadhi ya Wananchi.Hayo ameyasema leo kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati la kujadili makisio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2020/2021 lililofanyika ofisi za Makao mapya ya H/Wilaya Kijiji cha Loto kata ya Dareda."Kupitia kikao hiki nawashukuru sana Viongozi na Wananchi wa Kijiji cha Gallapo na Endanoga na kata kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi kuwasidia wenzao,kuwapeleka hospitali, kuwahifadhi, na kujenga mahema kwa watu waliopatwa na janga la upepo mkali siku ya jpili jioni ushirikiano huo naupongeza ni mfano wa kuigwa" amesisitiza Mkuu wa Wilaya,Aidha ametoa wito kwa wazazi kuchukua tahadhali kwa watoto wao wasikaribie na maji hasa kipindi hiki cha Mvua nyingi Wilayani Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.