Mkurugenzi Mtendaji wa Halashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Iddi Malinga ameitaka jamii kufanya kazi kwa bidii na kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kujiletea Maendeleo.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi huyo wakati alipotembelea ujenzi wa Madarasa 4, ofisi 2 na choo cha matundu 12 katika shule Mpya ya Sekondari ya Matufa. na kuwaahidi kuwapatia Bati za kuezekea jengo hilo bure "Fanyeni kazi kwa bidii kisha kila mmoja ashiriki ujenzi wa madarasa katika shule hii." Mkurugenzi alisistiza. Aidha Mkurugenzi Mtendaji ametembelea ujenzi wa Hostel ya kidato ya kidato cha tano na ujenzi wa madarasa 2 na ukarabati wa madarasa 3 kwa ajili ya kidato cha tano na tatu Shule ya Sekondari Mbugwe iliyoko kata ya Mwada Tarafa ya Mbugwe na kuwasisitiza Viongozi kusimamia ujenzi huo, na wananchi kuendelea kuchangia shule hiyo kwa hali na mali ili Watoto waweze kupata Elimu Bora kwa maisha yao ya Baadae
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.