Mbunge wa Jimbo la Babati Vijiji Mhe. Jitu Soni amewataka wananchi katika jimbo lake kumalizia vyumba vya madarasa ifikapo tarehe 8/01/2018 wanafunzi wote waliopangwa kuanza kidado cha kwanza waingie madarasani Mbunge amesema hayo wakati wa ziara yake yeye na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Nicodemus Tarmo aliyoifanya katika Kata za Mamire, Gallapo Endakiso na Qash kutembelea na kukagua shule za Kata zilizomo kwenye kata hizo. "Fanyeni kazi kwa bidii ili kumaliza ujenzi wa madarasa watoto waingie madarasani ifikapo tarehe 8/01/2017" Mbunge alisisitiza. Aidha wajumbe wa Serikali za vijiji wamesisitizwa kukusanya michango ya ujenzi kwa kila mwananchi bila kuangalia Cheo au kabila ili kumalizia ujenzi wa madarasa hayo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.