Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoa wa Manyara imeunda timu ya ufuatiliaji mapato ili kuhakikisha vyanzo vyote vilivyokisiwa kwenye bajeti 2022/2023 vinakusanywa ipasavyo na kwa wakati. Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Ndg Anna Mbogo ameunda timu hiyo yenye makundi matatu kupitia vyanzo vyote kwenye vijijji 102 kata 25 kuhakikisha wanakusanya mapato kwa kushirikiana na watendaji wa Vijiji.Timu hiyo inaenda kuongeza nguvu na msukumo mkubwa kwa mawakala wanaoendelea kukusanya mapato. Kiongozi huyo amesema fedha zitakazo patikana zitasaidia kukamilisha miradi ya Elimu,Afya na kilimo na akaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa timu hiyo na kulipa mapato ya serikali kwa wakati. Timu hiyo imeanza kazi kwa kwenda vijijini kukusanya mapato na imeonesha mafanikio makubwa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.