Wananchi wametakiwa kupima mara kwa mara afya zao ili kujikinga na magonjwa mbalimbali. Hayo ameyasema Mgeni Rasmi Mhe Mariam Kwimba Diwani wa Viti Maalum Kata ya Magugu kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ukumwi Duniani iliyofanyika katika
kata ya Magugu Kijiji cha Magugu. "kila mtu lazima ajiwekee utaratibu wa kupima afya yake kila mara ili kujikinga na magonjwa mbalimbali" alisisitiza Kiongozi huyo .Katika maadhimisho hayo shughuli za mbalimbali zilifanyika kama vile uzinduzi wa kampeini ya Vitamin A, dawa ya Minyoo na lishe kwa watoto chini ya mwaka 5,upimaji wa hiari wa VVU na Ukimwi na Ukusanyaji wa Damu salama. Aidha shuhuda mbalimbali zilitolewa juu ya kujikinga na VVU na Ukimwi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.