Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu amewashukuru Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kujiletea maendeleo.Mkuu wa Wilaya amesema hayo leo katika Mkutano wa pili wa Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati uliofanyika katika Ukumbi wa H/Wilaya ya Babati."Nawashukuru sana wananchi wa H/Wilaya ya Babati kwa kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo nawaomba jitihada hizo ziendelee". Amesisitiza Kiongozi huyo .Aidha ameipongeza Serikali kuu kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa. Pia Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Ndg Hamis Malinga kufuatilia fedha za maendeleo ambazo hazijaletwa kutoka kwenye mamlaka nyingine.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.