Mwenyekiti wa Ukombozi VICOBA Ndg. Rabieth Mulemba wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amewaomba wafanyakazi kujiunga na VICOBA kwa ajili ya kuendeleza miradi yao ili kujiletea maendeleo. Mwenyekiti huyo ameyasema hayo wakati wa kugawana hisa za wajumbe kwa mwaka 2017 na kuanza usajili mpya kwa mwaka 2018 na kusisitiza wajumbe kuzingatia kanuni na taratibu za kikundi hicho cha VICOBA.Kikundi cha Ukombozi VICOBA kina jumla ya wanachama 30, ambao wamewekaza hisa zao kuanzia Januari 2017 kila hisa Tsh.30,000 na wameweza kukusanya Jumla ya Hisa zote Tsh 41,880,000 na kutengeneza faida ya Tsh 12,115,995 ambapo kwa mwaka 2017 hisa moja imezaa Tsh.4,339.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.