Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Festo Dungange ameridhishwa na ubora na Matumizi ya fedha Tsh 470 Million zilizotolewa na Serikali katika ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Sarame. Mhe. Dungange ameyasema hayo leo Shuleni Sarame Ktk ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo Ktk H/ Wilaya ya Babati." Nawapongeza sana Viongozi na Watumishi wa H/ Wilaya ya Babati Kwa ujenzi na ubora wa majengo Ktk Shule hii ya Sarame, Nimekagua nimeridhika Shule imejengwa Kwa ubora unaotakiwa" amesisitiza kiongozi huyo.Amesema Halmashauri iendelee kutenga na kutoa fedha Kwa ajili ya ukamilishaji na Wizara itaendelea kumuomba Mhe. Rais ili atoe fedha za kuendeleza ujenzi Mradi huo. Naye Mbunge wa Babati Vijiji Mhe. Daniel Sillo ameomba Shule hiyo ijengewe mabweni kwani watoto wanatoka mbali na Barabara kutoka Barabara kuu iendayo Arusha kuelekea katika Shule hiyo itengenezwe. Shule hiyo mpya iliyoka Kata ya Magugu H/ Wilaya ya Babati inajengwa na Serikali kupitia mradi wa SEQUIP .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.